UHURU FM
DC Gairo aamuru kukamatwa viongozi waliokula fedha za ujenzi wa sekondari ya kata Idibo

MKUU wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe ameagiza kukamatwa kwa viongozi wote waliofuja shilingi milioni 32 za ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Idibo. Kauli hiyo ameitoa leo wakati alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa shule hiyo lililokwenda sambamba na ugawaji wa mabati na vifaa mbali mbali kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Kituo cha Polisi Idibo.

Mhe. Mchembe aliwaomba TAKUKURU kuwakamata viongozi wote wanaosimamia ujenzi wa shule ili waweze kuhojiwa matumizi ya pesa na wizi uliotokea tokea kuanza kwa ujenzi huo.

"Nimepokea taarifa ya Kamati ya Ujenzi ambayo imebaini wizi wa shilingi milioni 12 na matumizi ya utata yenye thamani ya shilingi milioni 20, hivyo ninawaagiza TAKUKURU na OCD ndani ya siku saba kuwakamata wale wote wanaohusika na sheria ichukue mkondo wake," alisema Mhe. Mchembe.

Aidha mpaka sasa japo kuna dosari Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata Idibo umemaliza madarasa 3, vyoo na jengo la utawala. Wakati huo huo Mhe. Mchembe alikabidhi msaada wa mabati 120 na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kupanua kituo cha Polisi Idibo kilichojengwa kwa nguvu za wananchi.

Katika hafla hiyo, Mhe. Mchembe aliyepokelewa na mwenyeji wake OCD - Gairo, Mratibu Mwandamizi Jeshi la Polisi, Ramadhani Kitantu, alitoa pongezi kwa Diwani Kata ya Idibo Mhe. Rajabu Mguhi na viongozi wake wote na wananchi wa Idibo kwa michango yao hadi boma kukamilika.

Mhe. Mchenbe aliwaomba wananchi washiriki kuchangia awamu ya pili ya umaliziaji bila kusahau nyumba za Polisi. Pia anakaribisha Wadau wengine wa maendeleo wenye Mapenzi mema na Gairo TUSHIRIKIANE.

Katibu Tawala Wilaya Bw. Adam John wakati wa ziara hizo alisisitiza wananchi kushirikiana na Serikali ili kujiletea Maendeleo yao. Pale ambapo kuna matatizo atahakikisha anayashughulikia ipasavyo kwa mujibu wa Sheria, Taratibu na Kanuni (STK).

Ndani ya mwaka mmoja tumefanikiwa kufungua Sekondari za Kata mbili ambazo ni Chagongwe na Chanjale. Kote huko watoto walikuwa wanatembea zaidi ya km 20 kwenda shule na maabara sita. Miradi yote ni nguvu za wananchi kwa zaidi ya asilimia 45 na fedha kutoka Serikali.

Pongezi kwa Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwajali watoto wa masikini huku pembezoni vijijini kabisa ambapo nao wanajisikia vizuri na wanajenga Uzalendo wa kuipenda nchi yao tangu wadogo.

Gairo ina kituo kimoja tu cha Polisi hivyo hiki kitakuwa cha pili. Kituo hiki kitahudumia Kata tano za Gairo na Kata jirani zaidi ya sita kutoka Wilaya ya Kilindi, Kiteto na Mvomero kwani kipo mpakani mwa Wilaya hizo.

RECENTS
MICHEZO
Kimbembe cha Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kinaendelea leo Jumamosi (Januari 13, 2018) kwa mechi nane za raundi ya 13 kupigwa katika viwanja nane tofauti.
January 13, 2018
Read More
KOREA Kaskazini imesema kuwa itatuma ujumbe wake katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi 2018 inayotarajiwa kufanyika Korea Kusini mnamo mwezi Februari kulingana na mji wa Seoul.
January 09, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amewasihi wananchi wa Tanzania kuendelea kuwaombea Dua na visomo mbali mbali Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wanaouawa wakilinda Amani katika nchini mbali mbali ikiwemo DRC Kongo.
January 22, 2018
Read More
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema wizara yake haina mpango wa kuongeza tena muda zoezi la utambuzi wa mifugo na kuwataka wafugaji popote walipo nchini kupaza sauti zao ili kuhakikisha kuwa ng’ombe na punda wote wamepigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.
January 20, 2018
Read More
ZOEZI la ugawaji wa Miguu ya kisasa ya bandia kwa watu wenye ulemavu wa Miguu awamu ya pili limeanza jana, ikiwa ni Kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kuwapatia Miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za uzalishaji Mali Kama awali ambapo imejidhihirisha kuwa RC Makonda akiahidi jambo analitimiza kwa vitendo na sio Siasa.
January 20, 2018
Read More
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume kusitisha usajili wa meli mpya hapa nchini mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.
January 19, 2018
Read More