UHURU FM
NECTA yatangaza matokeo ya mititahani ya upimaji darasa la nne na kidato cha pili

BARAZA la Mitihani la Taifa-NECTA, limetangaza matokeo ya mitihani ya Upimaji wa Darasa la Nne pamoja na Kidato cha Pili iliyofanyika Novemba 22 na 23 mwaka jana, huku likisema idadi kubwa ya wanafunzi wamefanya vyema katika Mitihani hiyo.

Akitangaza matokeo hayo leo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dokta CHARLES MSONDE, amesema, Wanafunzi Milioni Moja na Elfu-86 na 156 waliofanya mtihani wa darasa la Nne wamefaulu kati ya Milioni Moja Laki Moja na Elfu-58 na 444.

Wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata Alama zenye Madaraja ya A,B,C na D wakati Wanafunzi Elfu-72 na 288 sawa na Asilimia 6.24 wamepata Alama daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha.

Kuhusu matokea ya upimaji wa Kidato cha Pili, Dokta MSONDE, amesema, Wanafunzi Laki 4, Elfu-33na 453 sawa na Asilimia 82.32 kati ya Laki 4, Elfu-86 na 742 wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea na Kidato cha Tatu.

 

RECENTS
MICHEZO
Kimbembe cha Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kinaendelea leo Jumamosi (Januari 13, 2018) kwa mechi nane za raundi ya 13 kupigwa katika viwanja nane tofauti.
January 13, 2018
Read More
KOREA Kaskazini imesema kuwa itatuma ujumbe wake katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi 2018 inayotarajiwa kufanyika Korea Kusini mnamo mwezi Februari kulingana na mji wa Seoul.
January 09, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amewasihi wananchi wa Tanzania kuendelea kuwaombea Dua na visomo mbali mbali Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wanaouawa wakilinda Amani katika nchini mbali mbali ikiwemo DRC Kongo.
January 22, 2018
Read More
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema wizara yake haina mpango wa kuongeza tena muda zoezi la utambuzi wa mifugo na kuwataka wafugaji popote walipo nchini kupaza sauti zao ili kuhakikisha kuwa ng’ombe na punda wote wamepigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.
January 20, 2018
Read More
ZOEZI la ugawaji wa Miguu ya kisasa ya bandia kwa watu wenye ulemavu wa Miguu awamu ya pili limeanza jana, ikiwa ni Kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kuwapatia Miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za uzalishaji Mali Kama awali ambapo imejidhihirisha kuwa RC Makonda akiahidi jambo analitimiza kwa vitendo na sio Siasa.
January 20, 2018
Read More
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume kusitisha usajili wa meli mpya hapa nchini mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.
January 19, 2018
Read More