UHURU FM
Tsvangira agusia uwezekano wa kujiuzulu

KIONGOZI wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe, Morgan Tsvangirai amedokeza kwamba anaweza kuachia hatamu za uongozi wa chama hicho cha Movement for Democratic Change, MDC.

Katika taarifa aliyoitoa jana, Tsvangirai alisema anaangalia uwezekano wa viongozi wakongwe wa chama hicho kujiengua ili vijana wajitokeze kuchukua nafasi zao.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 65 amekuwa akipambana na saratani ya utumbo, na tangu kugunduliwa kwa ugonjwa huo mwaka 2016, ametumia muda wake mwingi nchini Afrika Kusini anakopata matibabu.

Tsvangira aliwahi kuwa waziri mkuu na mwenyekiti wa vyama vya wafanyakazi, na ni miongoni mwa watu wanaojulikana sana nchini Zimbabwe.

Yeye amekuwa mwenyekiti wa chama cha MDC tangu kiliupoundwa mwaka 1999.

Dokezo la kujiuzulu kwake limetolewa wakati Zimbabwe ikijiandaa kufanya uchaguzi wa rais na wabunge baadaye mwaka huu.

Source: DW

RECENTS
MICHEZO
Kimbembe cha Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kinaendelea leo Jumamosi (Januari 13, 2018) kwa mechi nane za raundi ya 13 kupigwa katika viwanja nane tofauti.
January 13, 2018
Read More
KOREA Kaskazini imesema kuwa itatuma ujumbe wake katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi 2018 inayotarajiwa kufanyika Korea Kusini mnamo mwezi Februari kulingana na mji wa Seoul.
January 09, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amewasihi wananchi wa Tanzania kuendelea kuwaombea Dua na visomo mbali mbali Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wanaouawa wakilinda Amani katika nchini mbali mbali ikiwemo DRC Kongo.
January 22, 2018
Read More
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema wizara yake haina mpango wa kuongeza tena muda zoezi la utambuzi wa mifugo na kuwataka wafugaji popote walipo nchini kupaza sauti zao ili kuhakikisha kuwa ng’ombe na punda wote wamepigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.
January 20, 2018
Read More
ZOEZI la ugawaji wa Miguu ya kisasa ya bandia kwa watu wenye ulemavu wa Miguu awamu ya pili limeanza jana, ikiwa ni Kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kuwapatia Miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za uzalishaji Mali Kama awali ambapo imejidhihirisha kuwa RC Makonda akiahidi jambo analitimiza kwa vitendo na sio Siasa.
January 20, 2018
Read More
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume kusitisha usajili wa meli mpya hapa nchini mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.
January 19, 2018
Read More