UHURU FM
Manispaa ya Ubungo Yapata Madarasa ya Kisasa

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, John Kayombo,leo amepokea jengo la kisasa lenye Madarasa mawili katika shule ya Sekondari Urafiki, Kata ya Ubungo, Jijini Dar es Salaam, kutoka kwa Kampuni ya Tanzania Steel Pipes Ltd.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Urafiki mbele ya Mgeni rasmi,  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori.

Kayombo aliomba msaada wa madarasa hayo mawili ya kisasa toka kwa kampuni ya Tanzania Steel Pipes Ltd baada ya kutembelea shule hiyo na kubaini uchakavu wa jengo lenye madarasa matano ambalo aliamuru libomolewe mara moja.

Aidha Kayombo amemhakikishia Mkuu wa wilaya kuwa Manisipaa yake itayatunza madarasa hayo na kusema tayari ameshatenga fedha kwa ajili ya ujenzi mwingine wa vyumba vitatu vya madarasa katika sehemu iliyo wazi shuleni hapo.

Kwa upande wake  Mhe. Kisare Makori baada ya kupokea Madarasa hayo amemshukuru Mkurugenzi wa Kampuni  ya Tanzania Steel Pipes Ltd, ndugu  Elly Bohela  kwa msaada na kuyataka makampuni mengine kuiga mfano huo.

 

RECENTS
MICHEZO
Kimbembe cha Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kinaendelea leo Jumamosi (Januari 13, 2018) kwa mechi nane za raundi ya 13 kupigwa katika viwanja nane tofauti.
January 13, 2018
Read More
KOREA Kaskazini imesema kuwa itatuma ujumbe wake katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi 2018 inayotarajiwa kufanyika Korea Kusini mnamo mwezi Februari kulingana na mji wa Seoul.
January 09, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amewasihi wananchi wa Tanzania kuendelea kuwaombea Dua na visomo mbali mbali Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wanaouawa wakilinda Amani katika nchini mbali mbali ikiwemo DRC Kongo.
January 22, 2018
Read More
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema wizara yake haina mpango wa kuongeza tena muda zoezi la utambuzi wa mifugo na kuwataka wafugaji popote walipo nchini kupaza sauti zao ili kuhakikisha kuwa ng’ombe na punda wote wamepigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.
January 20, 2018
Read More
ZOEZI la ugawaji wa Miguu ya kisasa ya bandia kwa watu wenye ulemavu wa Miguu awamu ya pili limeanza jana, ikiwa ni Kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kuwapatia Miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za uzalishaji Mali Kama awali ambapo imejidhihirisha kuwa RC Makonda akiahidi jambo analitimiza kwa vitendo na sio Siasa.
January 20, 2018
Read More
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume kusitisha usajili wa meli mpya hapa nchini mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.
January 19, 2018
Read More