UHURU FM
CHADEMA Yachafuka baada ya Lowasa Kumtembelea JPM

Hali ya wasiwasi imetanda ndani ya Chama Cha Democrasia na Maendeleo-CHADEMA, baada ya Baraza la Vijana la Chadema-Bavicha, kujitokeza leo mbele ya waandishi wa habari na kushutumu hatua ya Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama hicho, EDWARD LOWASSA, kumpongeza Rais JOHN MAGUFULI

Katika mkutano na waandishi wa habari, Katibu wa Bavicha, JULIUS MWITA, amehoji ni wapi LOWASSA anapata ujasiri wa kumpongeza Rais wakati nchi inakabiliwa na matukio mengi ya Uvunjaji wa haki za Binadamu.

MWITA amesema kitendo cha LOWASSA kumpongeza Rais MAGUFULI kimewasikitisha hasa kutokana na mazingira ya kisiasa yalivyo hapa nchini.

Juzi, LOWASSA alikutana na kufanya mazungumzo na Rais MAGUFULI Ikulu jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, alimpongeza kwa kazi nzuri anayofanya ya kuwaletea maendeleo ya haraka Watanzania.

 

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More