UHURU FM
Bomba la Gesi Kikwazo cha Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Mtwara

Bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka mkoani Mtwara kwenda jijini Dar es salaam limeanza kuleta utata baada ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA) kulihofia kutokana na kupita uwanja wa ndege.

Bomba hilo linapita katika hifadhi ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara ambao uko katika mpango wa kuupanua ili kuendana na mahitaji ya usafiri wa anga  baada ya TAA kuanza utaratibu wa kuupanua uwanja huo.

Hayo yamebainika baada ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa kutembelea uwanja huo na kuliagiza Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) pamoja na TAA kukaa na kuona ni kwa namna gani wataliondoa bomba hilo ambalo limeonekana kukwamisha shughuli za upanuzi wa uwanja.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Uwanja wa Ndege Mtwara, Daimon Mwakosya amesema katika mradi wa kupanua kiwanja hicho na kufikia code 4E na kuwa na uwezo wa kuhudumia ndege aina ya A340-200 na familia hiyo pamoja na Fire Cat 8.

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More