UHURU FM
VPL Kutimua Vumbi Wikiendi hii

Kimbembe cha Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kinaendelea leo Jumamosi (Januari 13, 2018) kwa mechi nane za raundi ya 13 kupigwa katika viwanja nane tofauti.

Mechi tatu kati ya nane zinafungua raundi ya 13 Jumamosi ambapo Lipuli FC itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar katika dimba la Samora mjini Iringa, wakati Stand United watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga.

Mbao FC waliotoka kuipiga Yanga 2-0 katika dimba la CCM Kirumba leo watasafiri hadi mkoani Mtwara kuwafuata Ndanda FC, mchezo utakaopigwa katika dimba la Nangwanda Sijaona.

Kesho Jumapili kutakuwa na patashika ya ‘Mbeya Derby’, pale ndugu wawili wa jiji la Mbeya, Tanzania Prisons na Mbeya City watakapoumana katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.

Ligi hiyo itaendelea Jumatatu kwa mchezo mmoja katika dimba la Sabasaba mjini Njombe, ambapo Njombe Mji watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar.

Mabingwa watetezi Yanga, watashuka dimbani siku ya Jumatano, Januari 17 katika dimba la Uhuru Dar es Salaam kuwavaa wachimba madini wa Mwadui FC.

Alhamisi, Januauri 18 ni vinara wa ligi hiyo, Simba SC watakaoshuka katika dimba la Uhuru Dar es Salaam kuvaana na matajiri wa Singida United, wakati Azam FC wakiwa ni wenyeji wa Majimaji FC mjini Songea siku hiyo hiyo.

RECENTS
MICHEZO
Kimbembe cha Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kinaendelea leo Jumamosi (Januari 13, 2018) kwa mechi nane za raundi ya 13 kupigwa katika viwanja nane tofauti.
January 13, 2018
Read More
KOREA Kaskazini imesema kuwa itatuma ujumbe wake katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi 2018 inayotarajiwa kufanyika Korea Kusini mnamo mwezi Februari kulingana na mji wa Seoul.
January 09, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amewasihi wananchi wa Tanzania kuendelea kuwaombea Dua na visomo mbali mbali Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wanaouawa wakilinda Amani katika nchini mbali mbali ikiwemo DRC Kongo.
January 22, 2018
Read More
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema wizara yake haina mpango wa kuongeza tena muda zoezi la utambuzi wa mifugo na kuwataka wafugaji popote walipo nchini kupaza sauti zao ili kuhakikisha kuwa ng’ombe na punda wote wamepigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.
January 20, 2018
Read More
ZOEZI la ugawaji wa Miguu ya kisasa ya bandia kwa watu wenye ulemavu wa Miguu awamu ya pili limeanza jana, ikiwa ni Kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kuwapatia Miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za uzalishaji Mali Kama awali ambapo imejidhihirisha kuwa RC Makonda akiahidi jambo analitimiza kwa vitendo na sio Siasa.
January 20, 2018
Read More
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume kusitisha usajili wa meli mpya hapa nchini mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.
January 19, 2018
Read More