UHURU FM
Uturuki Yaua Wapiganaji 260 wa Kikurdi nchini Syria

Uturuki imewauwa Wapiganaji 260 wa Kikurdi nchini Syria na Wanamgambo wa Kundi linalojiita Dola la Kiislamu- IS katika siku yake ya Nne ya operesheni ya eneo la Afrin Kaskazini mwa Syria lililo na Wakurdi wengi

 Rais wa Marekani, DONALD TRUMP, anapanga kuzungumzia suala hilo na mwenzake wa Uturuki TAYYIP ERDOGAN katika mazungumzo ya Simu kuhusu operesheni hiyo ya Uturuki dhidi ya wapiganaji wanaoungwa mkono na Marekani wa Kundi la Kikurdi la YPG.

 Rais wa Ufaransa EMMANUEL MACRON, pia ameelezea wasiwasi wake, Saa chache baada ya Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uturuki, kusema Uturuki inataka kuepuka makabiliano yoyote na Marekani, Urusi au Wanajeshi wa serikali ya Syria wakati wa operesheni hiyo, lakini itafanya chochote kinahohitajika kwa ajili ya usalama wake.

SOURCE:DW

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More