UHURU FM
Rais TFF Atoa Pole kwa Familia ya Kocha wa Mwadui alyefariki dunia

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania-TFF, Wallace Karia, amepokea kwa huzuni na mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Mwadui FC, Jumanne Ntambi kilichotokea usiku wa kuamkia leo Mkoani Shinyanga.

Taarifa ya TFF imesema Rais KARIA kwa niaba ya TFF, ametoa pole kwa familia ya Kocha huyo, Timu ya Mwadui FC, Wanafamilia wa Mpira wa Miguu, Ndugu, Jamaa pamoja na Marafiki.

Kocha NTAMBI hakuweza kuhudhuria mazoezi ya Mwadui yaliyofanyika jana kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Shinikizo la Damu.

Enzi za uhai wake Ntambi aliwahi kufundisha timu za Kahama United ya Shinyanga, Mlale JKT ya Ruvuma, Panone ya Kilimanjaro, Igembe Nsabo na mpaka mauti yanamkuta alikuwa akiifundisha Mwadui ya Shinyanga akiwa Kocha Msaidizi.

Wakati huo huo, Rais KARIA pia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya aliyekuwa Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba ISMAIL SUMA aliyefariki Dunia nchini Burundi.

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More