UHURU FM
Dkt. Mwakyembe atoa salamu za pole kifo cha Jumanne Ntambi

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amepokea kwa majonzi taarifa ya kifo cha Kocha Msaidizi wa timu ya  Mwadui FC Ndg. Jumanne Ntambi Kilichotokea  usiku wa tarehe 23 Januari, 2018 mkoani Shinyanga.

Dkt. Mwakyembe amesema kifo chake kimeacha pengo kubwa siyo tu kwa klabu ya Mwadui bali kwa sekta ya michezo ambayo marehemu aliitendea haki kutokana na umahiri wake katika kufundisha soka.

Dkt. Mwakyembe ametoa pole kwa familia ya marehemu, Uongozi wa Klabu ya Mwadui, Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Nchini (TAFCA), Shirikisho la   Mpira wa Miguu nchini (TFF), Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Wachezaji na Mashabiki wa Klabu ya Mwadui, ndugu, jamaa, marafiki na wanamichezo wote nchini na kuwaombea Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Wakati wa uhai wake marehemu Ndg. Ntambi alifundisha vilabu vya Kahama United ya Shinyanga, Mlale JKT ya Ruvuma, Panone ya Kilimanjaro, Timu ya Mkoa wa Shinyanga na Igembe Nsabo.  Hadi anafikwa na umauti marehemu Ntambi alikuwa akiifundisha timu ya Mwadui FC ya Shinyanga akiwa kama kocha msaidizi.

 

                           

Imetolewa na:

Lorietha Laurence

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.

24/01/2018.

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More