UHURU FM
Waasi S.Kusini Wataka Malipo Kuwaachia Marubani wa Kenya

Afisa wa kundi la waasi Sudan kusini amepuuzilia mbali taarifa kuwa wameitisha $200,000 ili wawaachilie huru marubani wawili wa Kenya wanaozuiwa katika eneo la Akobo, kaskazini mwa jimbo la Upper Nile.

Waasi hao waliwazuia marubani hao wawili baada ya ndege yao kuanguka, na kusababisha kifo cha mtu mmoja na ng'ombe kadhaa.

Hatahivyo waasi hao wanasema wanachotaka ni kulipwa fidia kwa hasara iliyotokana na vifo hivyo.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka televisheni inayomilikiwa na serikali, Utawala wa rais Salva Kiir Serikali ya Sudan kusini imewataka wawachilie marubani hao pasi masharti yoyote.

Taarifa ilisema kuwa waziri wa uchukuzi John Luke Jok ametuma kikosi kuchunguza ni nini kilichosababisha ajali hiyo ya ndege.

Gazeti la Sudan Tribune linaripoti kuwa Kanali Lam Paul Gabriel katika mahojiano na gazeti hilo Jumatano, alikana taarifa za vyombo vya habari kuwa gavana aliyeteuliwa wa waasi Koang Rambang aliitisha kikombozi ili kuwaachilia marubani hao wa Ken

Kanali Lam alithibitisha kuwa wanawazuia marubani hao tangu ndege hiyo ilipoanguka Januari 9 lakini alikana kuwa wametekwa na vikosi vya waasi wa SPLA-IO, linaripoti Sudan Tribune.

Mtu mmoja aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakatindege hiyo ilipoanguka.

Waasi hao wanaomtii aliyekuwa makamu wa kwanza rais Riek Machar wamesema hawatowaachilia raia hao wawili wa Kenya hadi familia iliopoteza jamaa yake katika ajali hiyo ilipwe fidia.

SOURCE:BBC

 

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More