UHURU FM
Waziri Mkuu Azitaka Nchi za Afrika Kuanza kujitegemea Kiuchumi

Waziri Mkuu, KASSIMA MAJALIWA, amesema nchi za Bara la Afrika zimeazimia kujiimarisha katika uzalishaji wa Umeme hadi Vijijini ili uweze kuleta maendeleo.

 Waziri Mkuu amesema hayo alipokuwa akizungumza baada ya mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliofanyika Mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia, ambapo katika Mkutano huo, amemwakilisha Rais JOHN MAGUFULI.

 Amesema nchi za Afrika zinatakiwa zijitegemee Kiuchumi, ambapo nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki na Jumuiya nyingine za Afrika zimefikia mapendekezo ya kuimarisha uzalishaji wa umeme.

Katika hatua nyingine, amesema mkutano huo umefanya mapitio ya mapendekezo ya namna nchi za Afrika zinavyoweza kupata mitaji kupitia michango ya nchi mbalimbali, ambapo kanuni ziliandaliwa ili kuwezesha kila nchi kuchangia katika mfuko Mkuu wa Umoja wa Afrika.

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More