UHURU FM
Ufafanuzi watolewa kuhusu Mamlaka ya Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa PALAMAGAMBA KABUDI, amefafanua kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana Mamlaka yote kisheria kutoa maagizo kwa mambo yote yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama nchi Huru.

Profesa KABUDI ametoa ufafanuzi huo leo Bungeni Mjini Dodoma kufuatia swali la nyongeza la Mbunge wa Wimbi, Zanzibar, JUMA KOMBO HAMADI aliteyataka kujua kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana mamlaka Kikatiba kutoa magizo kwa Waziri kutoka serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Amesema katika mambo yote yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mkuu wa nchini ni mmoja ambaye ni Rais JOHN MAGUFULI na yeye pekee ndiye Amiri Jeshi Mkuu na hakuna mtu yeyote wa kuamuru majeshi ya Tanzania isipokuwa yeye.

Aidha, Profesa KABUDI, amebainisha kuwa, Rais wa Zanzibar ni Mkuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwenye hadhi ya Rais kwa mambo yote yasiyokuwa ya Muungano pia ni Mjumbe rasmi wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nafasi yake.

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More