UHURU FM
Masoko ya hisa duniani yaporomoka na kusababisha mhemko kwa wawekezaji

HALI ya taharuki imeyakumba masoko ya hisa duniani leo ambapo mabara Asia na Ulaya yameshudia hasara zilizovunja rekodi kwenye masoko ya hisa ya Marekani mnamo wakati wawekezaji wa wakiweweseka kuhusiana na matarajio ya kupandishwa kwa viwango vya riba nchini Marekani kufuatia miezi kadhaa ya faida.

Mporomoko huo ulianza Ijumaa iliopita ilipobainika kuwa mfumo wa bei utaongezeka mwaka huu, na kwamba benki kuu ya Marekani italaazimika kupandisha gharama za ukopaji haraka zaidi kuliko ilivyotarajiwa.

Soko la hisa na New York la Dow Johns limeshuhudia mporomoko mkubwa zaidi wa siku moja wa hisa zake jana Jumatatu kwa kupoteza asilimia 4.6 ya thamani ya hisa zake.

Masoko ya hisa ya Ulaya yalipunguza faida zake leo na kusimama kwa asilimia 2.5, ikilinganishwa na viwango vya mwishoni mwa Jumatatu.

Source: DW

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More