UHURU FM
Katibu Mkuu UN aitaka Maldives kuondoa hali ya hatari

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameitaka serikali ya Maldives kuondoa hali ya hatari na kuhakikisha usalama wa raia wake wakiwemo watumishi wa idara ya mahakama.

Wito huo umekuja baada ya rais wa Maldives Abdullah Yameen, kutangaza hali ya hatari na vikosi vyake vya usalama kuivamia mahaka ya juu.

Jaji Mkuu wa mahakama hiyo pamoja na jaji mwingine walikamatwa pia. Taarifa iliyotolewa na msemaji wake Stephane Dujarric imesema kuwa Guterres anaisihi serikali ya Maldives kuheshimu katiba na utawala wa sheria kuondoa amari ya hali ya hatari haraka iwezekanavyo na kuchukuwa hatua zote kuhakikisha usalama wa watu nchini humo.

Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi kuhusu hali inayojitokeza nchini Maldives na hasa tangazo la hali ya hatari na hatua ya vikosi vya usalama kuingia katika eneo la mahakama.

Katika hotuba yake kwa taifa rais Yameen aliwatuhumu majaji kwa kuwa sehemu ya njama ya kumpindua.

Source: DW

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More