UHURU FM
Asilimia moja ya Idadi ya Watanzania wana ugonjwa wa Akili

Licha ya Serikali kueleza kutotambua idadi kamili ya wagonjwa wa Akili nchi nzima, inakadiriwa kuwa wagonjwa wa Akili ni Asilimia moja ya idadi ya Watanzania, takribani Milioni-50.

Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dokta FAUSTINE NDUGULILE, ametaja takwimu hizo Bungeni Mjini Dodoma kuwa Tanzania itakuwa na wastani wa takribani watu Laki Tano ambao ni wagonjwa wa Akili.

Amesema kati ya kadirio la Wagonjwa Laki Tano ni Asilimia 48 tu ndio wanafika kwenye Vituo vya kutolea huduma za Afya, Asilimia 24 wanapelekwa kwa Waganga wa Kienyeji, wakati Asilimia iliyobaki wanapelekwa katika huduma za kiroho na wachache ndiyo wanazunguka Mitaani.

Naibu Waziri, NDUGULILE, alikuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Morogoro Kusini, PROSPER MBENA, aliyetaka kujua ni kwa nini Serikali haina utaratibu wa kuchukua wagonjwa wa Akili wanaozunguka Mitaani

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More