UHURU FM
RC Geita,Awataka Wananchi kutoa Ushirikiano kwa Wataalamu wa Tathmini

Mkuu wa Mkoa wa Geita, ROBERT GABRIEL, amewataka wananchi wa Mkoa huo kutoa ushirikiano kwa wataalamu wanaopita kila Kaya kufanya utafiti na tathmini ya Uzazi, Unyonyeshaji, Afya, Uraia, Ulemavu, mapato na matumizi ya Kaya.

GABRIEL amesema utafiti huo utasaidia kubainisha hali ya umaskini katika Kaya ambao utasaidia pia serikali na wadau wa maendeleo kutimiza malengo mbalimbali ya maendeleo.

Madhumuni ya utafiti huo katika Kaya binafsi Tanzania Bara wa mwaka 2017/2018 ni kutoa takwimu za hali ya umasikini na nyingine ili kutathmini hatua stahiki za kutimiza malengo ya Kitaifa na Kimataifa.

Kata 34, Vijiji 34, Mitaa na Vitongoji 34 Mkoani Geita vinafanyiwa utafiti huo.

Naye Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, DOUGLAS MASANJA, amesema utafiti huo ambao unafanyika nchi nzima tangu Disemba Mosi mwaka jana, utakamilika mwezi Novemba mwaka huu.

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More