UHURU FM
UhakikI wa Madai ya Watumishi wa Umma wakamilika,Kulipwa kwa Mkupuo

Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.

Madai hayo yanayostahili kulipwa yanajumuisha shilingi Bilioni-16.25 kwa Walimu 15,919 na shilingi Bilioni-27 kwa watumishi wasiokuwa Walimu 11,470.

 Akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta PHILIP MPANGO, amesema madai yanayostahili kulipwa malipo ya madai mengine yana zaidi ya miaka Kumi na Majina yake yatatangazwa kwenye Magazeti kuanzia kesho.

Kiasi hicho cha fedha ni baada ya uhakiki wa madeni ambapo madai ya watumishi 27,389 kati ya Watumishi 82,111 yenye jumla ya shilingi Bilioni-43.3 ikiwa ni Asilimia 34 ya madai yote ya shilingi Bilioni-127.6 yameonekana ni sahihi na yanastahili kulipwa bila marekebisho.

 Kutokana na uhakiki huo ikiwemo kuwaondoa kwenye mfumo wa malipo ya Mishahara watumishi Hewa, vyeti feki na wasio na sifa na uhakiki wa madai ya malimbikizo ya mishahara, serikali imeokoa zaidi ya shilingi Bilioni-84 sawa na Asilimia 66 ya madai yote ya malimbikizo ya awali.

 

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More